Luke 8:19-21

19 aWakati mmoja mama yake Isa na ndugu zake walikuja kumwona, lakini hawakuweza kumfikia kwa sababu ya msongamano wa watu. 20 bMtu mmoja akamwambia, “Mama yako na ndugu zako wako nje wanataka kukuona.”

21 cIsa akamjibu, “Mama yangu na ndugu zangu ni wale wote wanaolisikia neno la Mungu na kulifanya.”

Isa Atuliza Dhoruba

(Mathayo 8:23-27; Marko 4:35-41)

Copyright information for SwhKC